5 Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli,Na nywele za kichwa chako kama urujuani,Mfalme amenaswa na mashungu yake.
6 Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu,Mapenzi katikati ya anasa!
7 Kimo chako kimefanana na mtende,Na maziwa yako na vichala.
8 Nilisema, Nitapanda huo mtende,Na kuyashika makuti yake.Maziwa yako na yawe kama vichala vya mzabibu,Na harufu ya pumzi yako kama mapera;
9 Na kinywa chako kama divai iliyo bora,Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu,Ikitiririka midomoni mwao walalao.
10 Mimi ni wake mpendwa wangu,Na shauku yake ni juu yangu.
11 Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani,Tufanye maskani katika vijiji.