1 Laiti ungekuwa kama ndugu yangu,Aliyeyanyonya matiti ya mamangu!Kama ningekukuta huko nje,Ningekubusu, asinidharau mtu.
2 Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu,Naye angenifundisha;Ningekunywesha divai iliyokolea,Divai mpya ya mkomamanga wangu.
3 Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu,Nao wa kuume ungenikumbatia.
4 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha,Hata yatakapoona vema?
5 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,Akimtegemea mpendwa wake?Nalikuamsha chini ya huo mpera;Huko mama yako alikuonea utungu,Aliona utungu aliyekuzaa.
6 Nitie kama muhuri moyoni mwako,Kama muhuri juu ya mkono wako;Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,Na wivu ni mkali kama ahera.Mwako wake ni mwako wa moto,Na miali yake ni miali ya Yahu.