1 Neno la BWANA lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli.
2 Sikieni haya, enyi wazee;Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi.Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu,Au katika siku za baba zenu?
3 Waarifuni watoto wenu habari yake,Watoto wenu wakawaambie watoto wao,Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.
4 Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.