6 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,Lenye nguvu, tena halina hesabu;Meno yake ni kama meno ya simba,Naye ana magego ya simba mkubwa.
7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
8 Ombolea kama mwanamwali avaaye maguniaKwa ajili ya mume wa ujana wake.
9 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.
10 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
11 Tahayarini, enyi wakulima;Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;Kwa ajili ya ngano na shayiri,Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
12 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;Naam, miti yote ya mashamba imekauka;Maana furaha imekauka katika wanadamu.