8 Ombolea kama mwanamwali avaaye maguniaKwa ajili ya mume wa ujana wake.
9 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.
10 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
11 Tahayarini, enyi wakulima;Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;Kwa ajili ya ngano na shayiri,Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
12 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;Naam, miti yote ya mashamba imekauka;Maana furaha imekauka katika wanadamu.
13 Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;Njoni mlale usiku kucha katika magunia,Enyi wahudumu wa Mungu wangu;Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
14 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,Na kumlilia BWANA,