7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,Nalimkumbuka BWANA;Maombi yangu yakakuwasilia,Katika hekalu lako takatifu.
8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongoHujitenga na rehema zao wenyewe;
9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;Nitaziondoa nadhiri zangu.Wokovu hutoka kwa BWANA.
10 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.