8 Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu.
9 Lakini, jihadharini: Huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
10 Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu?
11 Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako.
12 Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo, na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo.
13 Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi.