43 Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?
44 Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
45 Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.”
46 Naye Maria akasema,“Moyo wangu wamtukuza Bwana,
47 roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
48 Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu.Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
49 Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu,jina lake ni takatifu.