25 Kisha Yesu akawaambia, “Mbona mu wapumbavu kiasi hicho na mioyo yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii?
26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu wake?”
27 Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.
28 Walipokikaribia kile kijiji walichokuwa wanakiendea, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea na safari;
29 lakini wao wakamsihi wakisema, “Kaa pamoja nasi, maana kunakuchwa, na usiku unakaribia.” Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao.
30 Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.