7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.”
8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa:‘Utamwabudu Bwana Mungu wako,na kumtumikia yeye peke yake.’”
9 Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa hekalu, akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini
10 kwa maana imeandikwa:‘Atawaamuru malaika wake wakulinde,’
11 na tena,‘Watakuchukua mikononi mwao,usije ukajikwaa mguu kwenye jiwe.’”
12 Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
13 Ibilisi alipokwisha mjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.