51 Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
52 Watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili yake. Lakini Yesu akawaambia, “Msilie, kwa maana mtoto hajafa, amelala tu!”
53 Nao wakamcheka kwa sababu walijua kwamba alikuwa amekufa.
54 Lakini Yesu akamshika mkono akasema, “Mtoto, amka!”
55 Roho yake ikamrudia, akaamka mara. Yesu akaamuru wampe chakula.
56 Wazazi wake walishangaa, lakini Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote hayo yaliyotendeka.