43 Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu. [
44 Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.]
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu. [
46 Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.]
47 Na jicho lako likikukosesha, lingoe! Afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
48 Humo wadudu wake hawafi, na huo moto hauzimiki.
49 “Maana kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto.