15 Maana akili za watu hawa zimepumbaa,wameyaziba masikio yao,wameyafumba macho yao.La sivyo, wangeona kwa macho yao,wangesikia kwa masikio yao,wangeelewa kwa akili zao,na kunigeukia, asema Bwana,nami ningewaponya.’
16 “Lakini heri yenu nyinyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
17 Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.
18 “Basi, nyinyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
19 Yeyote asikiaye neno juu ya ufalme wa Mungu bila kuelewa, ni kama zile mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake.
20 Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye neno hilo na mara akalipokea kwa furaha.
21 Lakini halishiki na mizizi ndani yake; huendelea kulizingatia neno hilo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya neno hilo, anakata tamaa mara.