2 akawaambia, “Nendeni hadi kijiji kilicho mbele yenu na mtamkuta punda amefungwa na mtoto wake. Wafungueni mkawalete kwangu.
3 Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji,’ naye atawaachieni mara.”
4 Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa na nabii yatimie:
5 “Uambieni mji wa Siyoni:Tazama, Mfalme wako anakujia!Ni mpole na amepanda punda,mwanapunda, mtoto wa punda.”
6 Hivyo, wale wanafunzi walikwenda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza.
7 Wakamleta yule punda na mtoto wake, wakatandika nguo zao juu yao na Yesu akaketi juu yake.
8 Umati mkubwa wa watu wakatandaza nguo zao barabarani, na watu wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani.