11 Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima,zote zitachakaa kama vazi.
12 Utazikunjakunja kama koti,nazo zitabadilishwa kama vazi.Lakini wewe ni yuleyule daima,na maisha yako hayatakoma.”
13 Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:“Keti upande wangu wa kulia,mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.”
14 Malaika ni nini ila roho wanaomtumikia Mungu na ambao hutumwa kuwasaidia wale watakaopokea wokovu?