3 Kila kuhani mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu zawadi na tambiko, na hivyo kuhani mkuu wetu lazima naye awe na kitu cha kutolea.
4 Kama yeye angekuwa wa hapa duniani, asingekuwa kamwe kuhani, kwani wako makuhani wengine wanaotoa sadaka kufuatana na sheria.
5 Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”
6 Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
7 Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari, hakungalikuwa na haja ya agano la pili.
8 Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema:“Siku zinakuja, asema Bwana,ambapo nitafanya agano jipyana watu wa Israeli na wa Yuda.
9 Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zaosiku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri.Hawakuwa waaminifu kwa agano langu;na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.