2 naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake.
3 Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, “Hawana divai!”
4 Yesu akamjibu, “Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado.”
5 Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.”
6 Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
7 Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu.
8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”