19 Vilevile, miongoni mwa wazawa wa Aroni, makuhani waliokuwa wanakaa katika mashamba waliyomiliki kwa pamoja nje ya miji yao, mlikuwa watu maalumu kwenye miji hiyo ambao waliwagawia sehemu zao za vyakula. Waliwapa sehemu kila mwanamume katika jamaa za makuhani, na kila mmoja aliyekuwa ameandikishwa kati ya Walawi.