1 Daudi aliwahesabu watu waliokuwa pamoja naye, akawagawanya katika vikosi vya maelfu chini ya makamanda wao; na vikosi vya mamia, navyo chini ya makamanda wao.
2 Daudi akalituma jeshi lake vitani katika vikosi vitatu: Theluthi moja chini ya Yoabu, theluthi ya pili chini ya Abishai mwana wa Seruya, nduguye Yoabu; na theluthi ya tatu chini ya Itai, Mgiti. Kisha mfalme Daudi akawaambia wote, “Mimi mwenyewe binafsi nitakwenda pamoja nanyi.”
3 Lakini watu wakamwambia, “Hutatoka. Maana, ikiwa tutakimbia, hawatajali juu yetu. Ikiwa nusu yetu watakufa, pia hawatajishughulisha juu yetu. Lakini wewe una thamani kuliko watu 10,000 miongoni mwetu. Hivyo inafaa wewe ubaki mjini na kutupelekea msaada ukiwa mjini.”
4 Mfalme akawaambia, “Lolote mnaloona ni bora kwenu, nitalitenda.” Hivyo, mfalme akasimama kando ya lango, huku jeshi lake likipita: Mamia na maelfu.