30 Mfalme akasema, “Kaa kando, na usimame hapo.” Basi, Ahimaasi akaenda kando na kusimama kimya.
31 Ndipo na yule Mkushi akafika; naye akasema, “Kuna habari njema kwako bwana wangu mfalme! Maana Mwenyezi-Mungu leo hii amekukomboa kutoka nguvu za wale wote walioinuka dhidi yako.”
32 Mfalme akamwuliza, “Je kijana Absalomu hajambo?” Mkushi akasema, “Maadui wako, bwana wangu mfalme, pamoja na wote wanaoinuka dhidi yako wakikutakia mabaya, wawe kama huyo kijana Absalomu.”
33 Hapo mfalme alishikwa na huzuni kuu, akapanda kwenye chumba kilichokuwa juu ya lango na kulia. Alipokuwa anapanda, akawa analia akisema, “Mwanangu Absalomu, mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako! Ole, Absalomu mwanangu! Mwanangu!”