1 Daudi alimwimbia Mwenyezi-Mungu maneno ya wimbo ufuatao siku ile Mwenyezi-Mungu alipomkomboa mikononi mwa adui zake, na mkononi mwa Shauli.
2 Alisema,“Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu,ngome yangu, na mkombozi wangu.
3 Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama;ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu,ngome yangu na kimbilio langu.Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili.
4 Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie,nami naokolewa kutoka kwa adui zangu.
5 “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira,mafuriko ya maangamizi yalinivamia;
6 kamba za kuzimu zilinizinga,mitego ya kifo ilinikabili.