3 Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama;ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu,ngome yangu na kimbilio langu.Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili.
4 Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie,nami naokolewa kutoka kwa adui zangu.
5 “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira,mafuriko ya maangamizi yalinivamia;
6 kamba za kuzimu zilinizinga,mitego ya kifo ilinikabili.
7 “Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu;nilimwita Mungu wangu.Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu,kilio changu kilimfikia masikioni mwake.
8 “Hapo, dunia ikatetemeka na kutikisika,misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka,kwani Mungu alikuwa amekasirika.
9 Moshi ulifuka kutoka puani mwake,moto uunguzao ukatoka kinywani mwake,makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.