8 yafaa watumishi wa mfalme walete mavazi safi ya kitani aliyovaa mfalme na farasi wake mwenyewe,
9 na mmoja wa washauri wako wa kuheshimika, ee mfalme, amvishe mtu huyo mavazi hayo ya kifalme, na kumwongoza mtu huyo akiwa amepanda farasi wako mpaka kwenye uwanja wa mji, huku anatangaza: ‘Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme amependa kumpa heshima.’”
10 Hapo mfalme akamwambia Hamani, “Fanya haraka! Chukua mavazi hayo na farasi, ukamtunukie heshima hii Mordekai, Myahudi ambaye hukaa penye lango la ikulu. Usiache kumfanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”
11 Basi, Hamani akachukua mavazi hayo na kumvisha Mordekai, akamtembeza kwenye uwanja wa mji akiwa juu ya farasi wa mfalme, huku anatangaza: “Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme amependa kumpa heshima.”
12 Kisha Mordekai akarudi kwenye lango la ikulu. Lakini Hamani akakimbilia nyumbani kwake, amejaa huzuni na amekifunika kichwa chake kwa aibu.
13 Huko akawasimulia Zereshi, mkewe, na rafiki zake wote mambo yote yaliyompata. Zereshi na hao rafiki zake wakamwambia: “Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kupoteza madaraka yako kwake ni wa kabila la Wayahudi, basi, hutamweza; atakushinda kabisa.”
14 Walipokuwa bado wanaongea hayo, matowashi wa mfalme wakafika hima kumchukua Hamani kwenda kwenye karamu ya Esta.