53 ukoo wa Barkosi, wa Sisera, wa Tema,
54 ukoo wa Nezia na wa Hatifa.
55 Koo za wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa, ukoo wa Sotai, wa Hasoferethi, wa Perudha,
56 ukoo wa Yaala, wa Darkoni, wa Gideli,
57 ukoo wa Shefatia, wa Hatili, wa Pokereth-hasebaimu na wa Ami.
58 Nao watumishi wote wa hekalu na wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa watu 392.
59 Watu wa miji ifuatayo, pia walirudi: Wa mji wa Tel-mela, wa Tel-harsha, wa Kerubu, wa Adani na wa Imeri, ila hawakuweza kuthibitisha kuwa walikuwa wazawa wa Waisraeli.