1 Sala ya nabii Habakuki:
2 Ee Mwenyezi-Mungu, nimesikia juu ya fahari yako,juu ya matendo yako, nami naogopa.Uyafanye tena mambo hayo wakati wetu;uyafanye yajulikane wakati huu wetu.Ukasirikapo tafadhali ukumbuke huruma yako!
3 Mungu amekuja kutoka Temani,Mungu mtakatifu kutoka mlima Parani.Utukufu wake umetanda pote mbinguni,nayo dunia imejaa sifa zake.
4 Mng'ao wake ni kama wa jua;miali imetoka mkononi mwakeambamo nguvu yake yadhihirishwa.