3 Mungu amekuja kutoka Temani,Mungu mtakatifu kutoka mlima Parani.Utukufu wake umetanda pote mbinguni,nayo dunia imejaa sifa zake.
4 Mng'ao wake ni kama wa jua;miali imetoka mkononi mwakeambamo nguvu yake yadhihirishwa.
5 Maradhi yanatangulia mbele yake,nyuma yake yanafuata maafa.
6 Akisimama dunia hutikisika;akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka.Milima ya milele inavunjwavunjwa,vilima vya kudumu vinadidimia;humo zimo njia zake za kale na kale.
7 Niliwaona watu wa Kushani wakiteseka,na watu wa Midiani wakitetemeka.
8 Ee Mwenyezi-Mungu, je, umeikasirikia mito?Je, umeyakasirikia maji ya bahari,hata ukaendesha farasi wako,na magari ya vita kupata ushindi?
9 Uliuweka tayari uta wako,ukaweka mishale yako kwenye kamba.Uliipasua ardhi kwa mito.