14 bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
15 “Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote:
16 Mtapata laana katika miji yenu na mashamba yenu.
17 Vikapu vyenu vya nafaka vitalaaniwa na vyombo vyenu vya kukandia mkate.
18 Watoto wenu watalaaniwa na mazao yenu ya nchi; mifugo yenu italaaniwa isiongezeke.
19 Mtalaaniwa mnapoingia na mnapotoka.
20 “Mwenyezi-Mungu atawaleteeni maafa, vurugu na kukata tamaa katika shughuli zenu zote mpaka mmeangamia upesi kwa sababu ya uovu wa matendo yenu na kwa sababu ya kumwacha Mwenyezi-Mungu.