19 Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha;aliwakataa watoto wake, waume kwa wake.
20 Akasema, ‘Nitawaficha uso wangunione mwisho wao utakuwaje!Maana wao ni kizazi kipotovu,watoto wasio na uaminifu wowote.
21 Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu,wamenikasirisha kwa sanamu zao.Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu,nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.
22 Hasira yangu imewaka moto,inachoma mpaka chini kuzimu,itateketeza dunia na vilivyomo,itaunguza misingi ya milima.
23 Nitarundika maafa chungu nzima juu yao,nitawamalizia mishale yangu.
24 Watakonda kwa njaa,wataangamizwa kwa homa kali.Nitapeleka wanyama wenye meno makali kuwashambulia,na nyoka wenye sumu wanaotambaa mavumbini.
25 Vita vitasababisha vifo vingi njena majumbani hofu itawatawala,vijana wa kiume na wa kike watauawahata wanyonyao na wazee wenye mvi.