9 kulingana na idadi ya watoto wa Mungu,lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake,hao alijichagulia kuwa mali yake.
10 Aliwakuta katika nchi ya jangwa,nyika tupu zenye upepo mkali.Aliwalinda na kuwatunza,aliwafanya kama mboni ya jicho lake.
11 Kama tai alindaye kiota chake,na kurukaruka juu ya makinda yake,akitandaza mabawa yake ili kuwashikilia,na kuwabeba juu ya mabawa yake.
12 Yeye Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwaongozana hapakuwa na mungu mwingine wa kumsaidia.
13 Aliwapitisha katika nyanda za juu za nchi,nao wakala mazao ya mashambani.Akawapa asali miambani waonjena mafuta kutoka mwamba mgumu.
14 Aliwapa siagi na maziwa ya mifugo,mafuta ya wanakondoo na kondoo madume,makundi ya mifugo ya Bashani na mbuzi.Aliwapa ngano nzuri kabisa na divai mpya wakanywa.
15 Watu wa Israeli walinona na kupiga mateke;walinenepa, wakawa na kitambi na kunawiri;kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba,wakamdharau Mwamba wa wokovu wao.