1 Hii ndiyo baraka ambayo Mose, mtu wa Mungu aliwatakia Waisraeli kabla ya kufariki kwake. Alisema:
2 Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai,alitutokea kutoka mlima Seiri;aliiangaza kutoka mlima Parani.Alitokea kati ya maelfu ya malaika,na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
3 Mwenyezi-Mungu aliwapenda watu wake;na huwalinda watakatifu wake wote.Hivyo, malaika wake walifuata nyayo zake,na kupata maagizo kutoka kwake.
4 Mose alituamuru tutii sheria;kitu cha thamani kuu cha taifa letu.