14 Walitangatanga barabarani kama vipofu,walikuwa wamekuwa najisi kwa damu,hata asiwepo mtu yeyote wa kuwagusa.
15 Watu waliwapigia kelele wakisema:“Tokeni, nendeni zenu enyi mlio najisi!Tokeni, tokeni, msiguse chochote.”Hivyo wakawa wakimbizi na kutangatanga;watu wa mataifa walitamka:“Hawa hawatakaribishwa kukaa kwetu!”
16 Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwatawanya,wala hatawajali tena.Makuhani hawatapata tena heshima,wazee hawatapendelewa tena.
17 Tulichoka kukaa macho kungojea msaada;tulikesha na kungojea kwa hamutaifa ambalo halikuweza kutuokoa.
18 Watu walifuatilia hatua zetu,tukashindwa kupita katika barabara zetu.Siku zetu zikawa zimetimia;mwisho wetu ukawa umefika.
19 Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai,walitukimbiza milimani,walituvizia huko nyikani.
20 Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea,yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu,yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi waketutaishi miongoni mwa mataifa.”