4 Kizazi chapita na kingine chaja,lakini dunia yadumu daima.
5 Jua lachomoza na kutua;laharakisha kwenda machweoni.
6 Upepo wavuma kusini,wazunguka hadi kaskazini.Wavuma na kuvuma tena,warudia mzunguko wake daima.
7 Mito yote hutiririkia baharini,lakini bahari kamwe haijai;huko ambako mito hutiririkiandiko huko inakotoka tena.
8 Mambo yote husababisha uchovu,uchovu mkubwa usioelezeka.Jicho halichoki kuona,wala sikio kusikia.
9 Yaliyokuwako ndio yatakayokuwako,yaliyotendeka ndio yatakayotendeka;duniani hakuna jambo jipya.
10 Watu husema, “Tazama jambo jipya,”kumbe lilikwisha kuwako zama za kale.