5 wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya mawe pamoja;wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia;
6 wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza;wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa;
7 wakati wa kurarua na wakati wa kushona;wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea;
8 wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia;wakati wa vita na wakati wa amani.
9 Mfanyakazi hufaidi nini kutokana na juhudi zake hizo?
10 Mimi nimeiona kazi ambayo binadamu amepewa na Mungu.
11 Mungu amekifanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Amempa binadamu hamu ya kujua mambo ya baadaye, lakini hajamjalia fursa ya kuelewa matendo yake Mungu tangu mwanzo mpaka mwisho.