13 lakini hakuna furaha kwa waovu. Wao watapita kama kivuli, maisha yao hayatakuwa marefu kwa sababu hawamchi Mungu.
14 Kuna jambo moja, bure kabisa nililoligundua hapa duniani: Watu wema hutendewa wastahilivyo waovu, nao waovu hutendewa wastahilivyo watu wema. Hili nalo nasema ni bure kabisa.
15 Basi, mimi nasisitiza kuwa mtu ni lazima afaidi raha, kwa kuwa hapa duniani hakuna kilicho kizuri zaidi kuliko kula na kunywa na kujifurahisha. Hayo ndio awezayo kufanya mtu anaposhughulika na kazi katika muda wa maisha yake aliyojaliwa na Mungu duniani.
16 Kila nilipojaribu kujua hekima na kuona yanayotendeka hapa duniani, niligundua kwamba unaweza kukaa macho mchana na usiku,
17 halafu niliona kazi yote ya Mungu ya kwamba mwanadamu hawezi kuelewa kazi inayofanyika duniani. Wenye hekima wanaweza kujidai eti wanajua, lakini, kwa kweli, hawajui.