1 Ole wao wanaopanga kutenda maovuwanaolala usiku wakiazimia uovu!Mara tu kunapopambazuka,wanayatekeleza kwani wanao uwezo.
2 Hutamani mashamba na kuyatwaa;wakitaka nyumba, wananyakua.Huwadhulumu wenye nyumba na jamaa zao,huwanyang'anya watu mali zao.
3 Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Ninapanga kuwaleteeni nyinyi maafa,ambayo kamwe hamtaweza kuyakwepa.Utakuwa wakati mbaya kwenu,wala hamtaweza kwenda kwa maringo.
4 Siku hiyo watu watawasimanga kwa wimbo,watalia na kuomboleza kwa uchungu, wakisema:‘Tumeangamia kabisa;Mwenyezi-Mungu amechukua nchi yetu,naam, ameiondoa mikononi mwetu.Mashamba yetu amewagawia waliotuteka.’”