1 Sikilizeni anachosema Mwenyezi-Mungu:“Wewe nabii, nenda ukailalamikie milima,navyo vilima visikie sauti yako.”
2 Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima,sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia!Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake.Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli.
3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Enyi watu wangu, nimewatendea nini?Nimewachosha kwa kitu gani?Nijibuni!
4 Mimi niliwatoa nchini Misri;niliwakomboa kutoka utumwani;niliwapeni Mose, Aroni na Miriamu kuwaongoza.
5 Enyi watu wangu,kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu,na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu.Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali.Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”