2 Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima,sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia!Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake.Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli.
3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Enyi watu wangu, nimewatendea nini?Nimewachosha kwa kitu gani?Nijibuni!
4 Mimi niliwatoa nchini Misri;niliwakomboa kutoka utumwani;niliwapeni Mose, Aroni na Miriamu kuwaongoza.
5 Enyi watu wangu,kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu,na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu.Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali.Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
6 Nimwendee Mwenyezi-Mungu na kitu gani,nipate kumwabudu Mungu aliye juu?Je, nimwendee na sadaka za kuteketezwa,nimtolee ndama wa mwaka mmoja?
7 Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwanikimtolea maelfu ya kondoo madume,au mito elfu na elfu ya mafuta?Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanzakwa ajili ya kosa langu,naam, mtoto wangukwa ajili ya dhambi yangu?
8 Mungu amekuonesha yaliyo mema, ewe mtu;anachotaka Mwenyezi-Mungu kwako ni hiki:Kutenda mambo ya haki,kupenda kuwa na huruma,na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako.