1 Ole wako mji wa mauaji!Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele,usiokoma kamwe kuteka nyara.
2 Sikia! Mlio wa mjeledi,mrindimo wa magurudumu,vishindo vya farasina ngurumo za magari!
3 Wapandafarasi wanashambulia,panga na mikuki inametameta;waliouawa hawana idadi,maiti wengi sana;watu wanajikwaa juu ya maiti!
4 Ninewi! Wewe umekuwa kama malaya.Umewashawishi watu, ewe binti wa uchawi,uliyeyafanya mataifa kuwa watumwa kwa umalaya wako,na watu wa mataifa kwa uchawi wako.