1 Kauli ya Mungu juu ya Ninewi. Kitabu cha maono ya Nahumu wa Elkoshi.
2 Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi;Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu;Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake,huwaka ghadhabu juu ya adui zake.
3 Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu,Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia.Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba;mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
4 Huikaripia bahari na kuikausha,yeye huikausha mito yote.Mbuga za Bashani na mlima Karmeli hunyauka,maua ya Lebanoni hudhoofika.
5 Milima hutetemeka mbele yake,navyo vilima huyeyuka;dunia hutetemeka mbele yake,ulimwengu na vyote vilivyomo.
6 Nani awezaye kuikabili ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu?Nani awezaye kustahimili ukali wa hasira yake?Yeye huimwaga hasira yake iwakayo kama moto,hata miamba huipasua vipandevipande.
7 Mwenyezi-Mungu ni mwema,yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu.Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.
8 Adui wakiivamia nchi kama mafuriko, yeye huwaangamiza;huwafuatia na kuwafukuza mpaka gizani.
9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu?Yeye atawakomesha na kuwaangamiza,wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.
10 Watateketezwa kama kichaka cha miiba,kama vile nyasi zilizokauka.
11 Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungualiyefanya njama za ulaghai.
12 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake:“Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu,wao wataangushwa na kuangamizwa.Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu,sitawateseni tena zaidi.
13 Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu,na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.”
14 Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi:“Hutapata wazawa kulidumisha jina lako.Sanamu zako za kuchonga na za kusubu,nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako.Mimi nitakuchimbia kaburi lako,maana wewe hufai kitu chochote.”
15 Enyi watu wa Yuda tazameni:Anakuja kutoka mlimani mtu anayeleta habari njema,mjumbe ambaye anatangaza amani.Adhimisheni sikukuu zenu, enyi watu wa Yuda,timizeni nadhiri zenu,maana waovu hawatawavamia tena,kwani wameangamizwa kabisa.