Nahumu 2 BHN

Kuanguka kwa Ninewi

1 Mwangamizi amekuja kukushambulia ee Ninewi.Chunga ngome zako!Weka ulinzi barabarani!Jiweke tayari!Kusanya nguvu zako zote!

2 Mwenyezi-Mungu anamrudishia Yakobo fahari yake,naam, anawapa tena Waisraeli fahari yao,ingawa wavamizi hawakuwaachia kitu,hata matawi yao ya mizabibu waliyakata.

3 Ngao za mashujaa wake ni nyekundu,askari wake wamevaa mavazi mekundu sana.Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto,yamepangwa tayari kushambulia;farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.

4 Magari ya farasi yanatimua mbio barabarani,yanakwenda huko na huko uwanjani.Yanamulika kama miali ya moto!Yanakwenda kasi kama umeme.

5 Sasa anawaita maofisa wake,nao wanajikwaa wanapomwendea;wanakwenda ukutani himahimakutayarisha kizuizi.

6 Vizuizi vya mito vimefunguliwa,ikulu imejaa hofu.

7 Mji uko wazi kabisa,watu wamechukuliwa mateka.Wanawake wake wanaomboleza,wanalia kama njiwa,na kujipigapiga vifuani.

8 Ninewi ni kama bwawa lililobomoka,watu wake wanaukimbia ovyo.“Simameni! Simameni!” Sauti inaita,lakini hakuna anayerudi nyuma.

9 “Chukueni nyara za fedha,chukueni nyara za dhahabu!Hazina yake haina mwisho!Kuna wingi wa kila kitu cha thamani!”

10 Mji wa Ninewi ni maangamizi matupu na uharibifu!Watu wamekufa moyo, magoti yanagongana,nguvu zimewaishia, nyuso zimewaiva!

11 Limekuwaje basi hilo pango la simba,hilo lililokuwa maficho ya wanasimba?Pamekuwaje hapo mahali pa simba,mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?

12 Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha,akawakamatia simba majike mawindo yao;ameyajaza mapango yake mawindo,na makao yake mapande ya nyama.

13 Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: Nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.

Sura

1 2 3