12 Ngome zako zote ni za tini za mwanzo;zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani.
13 Tazama askari wako:Wao ni waoga kama wanawake.Milango ya nchi yako ni wazi mbele ya adui zako;moto umeyateketeza kabisa makomeo yake.
14 Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa;imarisheni ngome zenu.Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga,tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!
15 Lakini huko pia moto utawateketezeni,upanga utawakatilia mbali;utawamaliza kama nzige walavyo.Ongezekeni kama nzige,naam, ongezekeni kama panzi!
16 Wafanyabiashara wako waliongezeka kuliko nyota;lakini sasa wametoweka kama panzi warukavyo.
17 Wakuu wako ni kama panzi,maofisa wako kama kundi la nzige;wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta,lakini jua lichomozapo, huruka,wala hakuna ajuaye walikokwenda.
18 Ewe mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala,waheshimiwa wako wamesinzia.Watu wako wametawanyika milimani,wala hakuna yeyote wa kuwakusanya.