16 Wafanyabiashara wako waliongezeka kuliko nyota;lakini sasa wametoweka kama panzi warukavyo.
17 Wakuu wako ni kama panzi,maofisa wako kama kundi la nzige;wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta,lakini jua lichomozapo, huruka,wala hakuna ajuaye walikokwenda.
18 Ewe mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala,waheshimiwa wako wamesinzia.Watu wako wametawanyika milimani,wala hakuna yeyote wa kuwakusanya.
19 Hakuna wa kuyapa nafuu majeraha yako,vidonda vyako ni vya kifo.Wote wanaosikia habari zako wanashangilia.Maana ni nani aliyeuepa ukatili wako usio na kikomo?