3 Wapandafarasi wanashambulia,panga na mikuki inametameta;waliouawa hawana idadi,maiti wengi sana;watu wanajikwaa juu ya maiti!
4 Ninewi! Wewe umekuwa kama malaya.Umewashawishi watu, ewe binti wa uchawi,uliyeyafanya mataifa kuwa watumwa kwa umalaya wako,na watu wa mataifa kwa uchawi wako.
5 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe;nitalipandisha vazi lako hadi kichwani,niyaache mataifa yauone uchi wako,tawala ziikodolee macho aibu yako.
6 Nitakutupia uchafu,na kukutendea kwa dharau,na kukufanya uwe kioja kwa watu.
7 Kisha wote watakaokuona watakukimbia wakisema,“Ninewi umeangamizwa,ni nani atakayeuombolezea?Nani atakayekufariji?”
8 Je, wewe Ninewi, ni bora kuliko Thebesi,mji uliojengwa kando ya mto Nili?Thebesi ulizungukwa na maji,bahari ilikuwa boma lake,maji yalikuwa ukuta wake!
9 Kushi ilikuwa nguvu yake;nayo Misri pia, tena bila kikomo;watu wa Puti na Libia waliusaidia!