8 Je, wewe Ninewi, ni bora kuliko Thebesi,mji uliojengwa kando ya mto Nili?Thebesi ulizungukwa na maji,bahari ilikuwa boma lake,maji yalikuwa ukuta wake!
9 Kushi ilikuwa nguvu yake;nayo Misri pia, tena bila kikomo;watu wa Puti na Libia waliusaidia!
10 Hata hivyo, ulichukuliwa mateka,watu wake wakapelekwa uhamishoni.Hata watoto wake walipondwapondwakatika pembe ya kila barabara;watu wake mashuhuri walinadiwa,wakuu wake wote walifungwa minyororo.
11 Ninewi, nawe pia utalewa;utamkimbia adui na kujaribu kujificha.
12 Ngome zako zote ni za tini za mwanzo;zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani.
13 Tazama askari wako:Wao ni waoga kama wanawake.Milango ya nchi yako ni wazi mbele ya adui zako;moto umeyateketeza kabisa makomeo yake.
14 Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa;imarisheni ngome zenu.Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga,tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!