1 Kusanyikeni, kusanyikeni enyi taifa la watu wasio na aibu,
2 kabla hamjapeperushwa mbali kama makapi,kabla haijawajia siku ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu,kabla haijawajia siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
3 Mtafuteni Mwenyezi-Mungu enyi wanyenyekevu wote nchini,enyi mnaozitii amri zake.Tafuteni uadilifu, tafuteni unyenyekevu;labda mtaiepa siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
4 Mji wa Gaza utahamwa,Ashkeloni utakuwa tupu.Wakazi wa Ashdodi watatimuliwa mchana,na wale wa Ekroni watang'olewa.
5 Ole wenu wakazi wa nchi za pwani,watu mnaoishi huko Krete!Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenuenyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia:Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja!
6 Nanyi nchi za pwani mtafanywa kuwa malisho;mtakuwa vibanda vya wachungajina mazizi ya kondoo.
7 Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda.Watachunga mifugo yao huko.Nyumba za mji wa Ashkelonizitakuwa mahali pao pa kulala.Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbukana kuwarudishia hali yao njema.
8 “Nimeyasikia masuto ya Moabuna dhihaka za Waamoni;jinsi walivyowasuta watu wangu,na kujigamba kuiteka nchi yao.
9 Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,mimi Mungu wa Israeli,Moabu itakuwa kama Sodomana Amoni itakuwa kama Gomora.Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi,zitakuwa ukiwa milele.Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara,watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”
10 Hayo yatakuwa malipo ya kiburi chao,kwa sababu waliwadhihaki na kujigambadhidi ya watu wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
11 Mwenyezi-Mungu atakuwa wa kutisha dhidi yao;miungu yote ya dunia ataikondesha.Mataifa yote duniani yatamsujudia;kila taifa katika mahali pake.
12 Nanyi watu wa Kushi piamtauawa kwa upanga wake.
13 Mwenyezi-Mungu atanyosha mkono wake kaskazini,na kuiangamiza nchi ya Ashuru.Ataufanya mji wa Ninewi kuwa ukiwa,kuwa mahali pakavu kama jangwa.
14 Makundi ya mifugo yatalala humo,kadhalika kila mnyama wa porini.Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake,bundi watalia kwenye madirisha yake,kunguru watalia kwenye vizingiti,maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu.
15 Je, huu ndio mji uliojivuna na kuishi kwa usalama,mji uliojisemea, “Ni mimi tu, hakuna mwingine!”Jinsi gani umekuwa mtupuna makao ya wanyama wa mwituni!Kila apitaye karibu atauzomea na kuudharau.