1 Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amenia, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa mfalme Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda:
2 Mwenyezi-Mungu asema:“Nitavifagilia mbali viumbe vyote duniani:
3 Wanadamu, wanyama, ndege wa anganina samaki wa baharini;vyote nitaviangamiza.Waovu nitawaangamiza kabisa;wanadamu nitawafagilia mbali duniani.
4 Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda,kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu.Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii,na hakuna atakayetambua jina lao.
5 Nitawaangamiza wote wanaosujudu juu ya paa,wakiabudu jeshi la mbinguni.Nitawaangamiza wale wanaoniabuduna kuapa kwa jina langu,hali wanaapa pia kwa jina la mungu Milkomu.
6 Nitawaangamiza wote walioniacha mimi Mwenyezi-Munguwote walioacha kunitafuta na kuniuliza shauri.”
7 Nyamazeni mbele ya Bwana Mwenyezi-Mungu,kwani siku ya Mwenyezi-Mungu iko karibu.Mwenyezi-Mungu ameandaa tambiko,nao aliowaalika amewateua.
8 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Katika siku ile ya karamu yangu,nitawaadhibu viongozi wa watu hao,kadhalika na wana wa mfalmepamoja na wote wanaoiga desturi za kigeni.
9 Siku hiyo nitawaadhibu wote:Wanaoruka kizingiti cha nyumba kama wapagani,wanaojaza nyumba ya bwana wao vitu vya dhuluma na wizi.
10 “Siku hiyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu,Kutasikika kilio kutoka Lango la Samaki,maombolezo kutoka Mtaa wa Pili,na mlio mkubwa kutoka milimani.
11 Lieni enyi wakazi wa Makteshi!Wafanyabiashara wote wameangamia,wote wapimao fedha wamefutiliwa mbali.
12 Wakati huo nitaupekua mji wa Yerusalemu kwa taa,nitawaadhibu wanaoishi wametulia kama machicha ya divai,wote ambao husema mioyoni mwao:‘Mwenyezi-Mungu hatafanya kitu: Chema au kibaya.’
13 Utajiri wao utanyakuliwa,na nyumba zao zitaachwa tupu!Watajijengea nyumba, lakini hawataishi humo.Watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake.”
14 Ile siku kubwa ya Mwenyezi-Mungu imekaribia,iko karibu na inakuja mbio.Mlio wa siku ya Mwenyezi-Mungu ni wa uchungu;hapo, shujaa atalia kwa sauti.
15 Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu,ni siku ya dhiki na uchungu,siku ya giza na huzuni;siku ya uharibifu na maangamizi,siku ya mawingu na giza nene.
16 Siku hiyo ni ya mlio wa tarumbeta ya vita,dhidi ya miji yenye ngome na kuta ndefu.
17 Kwa kuwa watu wamemkosea Mwenyezi-Mungu,yeye atawaletea dhiki kubwa,hivyo kwamba watatembea kama vipofu.Damu yao itamwagwa kama vumbi,na miili yao kama mavi.
18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoakatika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.Kwa moto wa wivu wakedunia yote itateketezwa.Kwa ukamilifu na kwa namna ya kutishaatawafanya wakazi wote duniani watoweke.