10 Hayo yatakuwa malipo ya kiburi chao,kwa sababu waliwadhihaki na kujigambadhidi ya watu wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
11 Mwenyezi-Mungu atakuwa wa kutisha dhidi yao;miungu yote ya dunia ataikondesha.Mataifa yote duniani yatamsujudia;kila taifa katika mahali pake.
12 Nanyi watu wa Kushi piamtauawa kwa upanga wake.
13 Mwenyezi-Mungu atanyosha mkono wake kaskazini,na kuiangamiza nchi ya Ashuru.Ataufanya mji wa Ninewi kuwa ukiwa,kuwa mahali pakavu kama jangwa.
14 Makundi ya mifugo yatalala humo,kadhalika kila mnyama wa porini.Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake,bundi watalia kwenye madirisha yake,kunguru watalia kwenye vizingiti,maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu.
15 Je, huu ndio mji uliojivuna na kuishi kwa usalama,mji uliojisemea, “Ni mimi tu, hakuna mwingine!”Jinsi gani umekuwa mtupuna makao ya wanyama wa mwituni!Kila apitaye karibu atauzomea na kuudharau.