3 Mkono wako wa kushoto u chini ya kichwa changu,na mkono wako wa kulia wanikumbatia.
4 Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu,msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,hadi hapo wakati wake utakapofika.
5 Ni nani huyu ajaye kutoka mbugani,huku anamwegemea mpenzi wake?Chini ya mtofaa, mimi nilikuamsha,pale ambapo mama yako aliona uchungu,naam, pale ambapo mama yako alikuzaa.
6 Nipige kama mhuri moyoni mwako,naam, kama mhuri mikononi mwako.Maana pendo lina nguvu kama kifo,wivu nao ni mkatili kama kaburi.Mlipuko wake ni kama mlipuko wa moto,huwaka kama mwali wa moto.
7 Maji mengi hayawezi kamwe kulizima,mafuriko hayawezi kulizamisha.Mtu akijaribu kununua pendo,akalitolea mali yake yote,atakachopata ni dharau tupu.
8 Tunaye dada mdogo,ambaye bado hajaota matiti.Je, tumfanyie nini dada yetusiku atakapoposwa?
9 Kama angalikuwa ukuta,tungalimjengea mnara wa fedha;na kama angalikuwa mlango,tungalimhifadhi kwa mbao za mierezi.