5 Wanaporukaruka kwenye vilele vya milima,wanarindima kama magari ya farasi,wanavuma kama mabua makavu motoni.Wamejipanga kama jeshi kubwatayari kabisa kufanya vita.
6 Wakaribiapo, watu hujaa hofu,nyuso zao zinawaiva.
7 Wanashambulia kama mashujaa wa vita;kuta wanazipanda kama wanajeshi.Wote wanakwenda mbele moja kwa moja,bila hata mmoja wao kubadilisha njia.
8 Hakuna amsukumaye mwenziwe;kila mmoja anafuata mkondo wake.Wanapita kati ya vizuizi vya silaha,wala hakuna kiwezacho kuwazuia.
9 Wanauvamia mji,wanapiga mbio ukutani;wanaziparamia nyumba na kuingia,wanapenya madirishani kama wezi.
10 Nchi inatetemeka mbele yao,mbingu zinatikisika.Jua na mwezi vyatiwa giza,nazo nyota zinaacha kuangaza.
11 Mwenyezi-Mungu anaamuru jeshi lake kwa sauti;askari wake ni wengi mno,wanaomtii hawahesabiki.2Siku ya Mwenyezi-Mungu kweli ni kuu na ya kutisha sana!Nani atakayeweza kuistahimili?