3 Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari,gharika ikanizunguka,mawimbi na gharika vikapita juu yangu.
4 Nilidhani kwamba nimetengwa nisiwe mbele yako;nisiweze kuliona tena hekalu lako takatifu.
5 Maji yalinizunguka na kunisonga;kilindi kilinifikia kila upande,majani ya baharini yakanifunika kichwa.
6 Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima,katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele.Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu,umenipandisha hai kutoka humo shimoni.
7 Roho yangu ilipoanza kunitoka,nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu,sala yangu ikakufikia,katika hekalu lako takatifu.
8 Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili,huutupilia mbali uaminifu wao kwako.
9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,nitakutolea sadaka,na kutimiza nadhiri zangu.Mwenyezi-Mungu, ndiye aokoaye.”